
amishna Msaidizi wa Uhifadhi – Kitengo cha Mawasiliano - TANAPA, Catherine Mbena.
-----------------------------
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limekanusha taarifa ilizoziita potofu kwenye mitandao ya kijamii kwamba limesitisha safari za kitalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kutokana na mvua.
“TANAPA inaufahamisha umma kuwa safari za kitalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti na hifadhi zingine zote hazijasitishwa - zinaendelea kama kawaida na kwa sasa vivuko vyote katika HIfadhi ya Taifa Serengeti vinapitika.
“Aidha, TANAPA inasisitiza madereva wa magari ya watalii kufuata maelekezo yote ya timu za uokoaji zilizopo katika vivuko vyote katika Hifadhi ya Serengeti,” TANAPA imeeleza katika taarifa yake kwa umma ya Machi 7, 2026, iliyosainiwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi – Kitengo cha Mawasiliano, Catherine Mbena.
No comments:
Post a Comment