NEWS

Monday, 30 March 2026

Waziri Nyansaho amsifu Prof. Muhongo kwa ushauri wa kuinua ufaulu wa wanafunzi Mara



Kutoka kushoto ni Waziri Dkt. Rhimo Nyansaho na Mbunge Prof. Sospeter Muhongo

Na Mwandishi Wetu
Musoma
-----------------

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amemsifu Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, kwa juhudi zake za kupendekeza mbinu za kuinua ufaulu wa wanafunzi mkoani Mara.

Akizungumza mjini Musoma hivi karibuni katika hafla ya kukabidhi saruji mifuko 6,000 kwa wabunge 12 wa mkoa huo, Waziri Nyansaho alisema Prof. Muhongo ni mfano wa kuigwa kwa kutoa mawazo ya kuboresha elimu.

“Profesa my brother (kaka yangu) huwa anafuatilia sana, anapenda kuonesha nini kifanyike… tuwe tunayachukulia kwa positive mind (mtanzamo chanya),” alisema Waziri Nyansaho.

Aliongeza kuwa haiwezekani kuzungumzia elimu kama mkombozi huku mkoa huo ukishika nafasi za mwisho kitaifa. “Tumeanza kushuka, lazima tutafute chanzo cha tatizo,” alisisitiza.

Takwimu zinaonesha ufaulu wa darasa la saba na kidato cha nne Mara umekuwa ukiporomoka katika miaka ya karibuni.

Mfano, mwaka 2025, mkoa wa Mara ulishika nafasi ya mwisho kati ya mikoa yote 26 ya Tanzania Bara katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba.

Miongoni mwa mapendekezo ya Muhongo ni kuitisha mikutano ya wadau kuanzia ngazi ya familia hadi mkoa ili kubaini chanzo na kupata suluhisho la kudumu la kushuka kwa ufaulu.

Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages