
F-15
Marekani imemuokoa rubani wa pili aliyepotea ndani ya Iran baada ya ndege ya kivita aina ya F-15 ya nchi hiyo kudunguliwa Ijumaa iliyopita kusini mwa Iran.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amethibitisha kuokolewa kwa rubani huyo kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social mapema leo Jumapili, baada ya Jeshi la Marekani kuendesha operesheni ya kimkakati ya uokoaji katika historia yake.
“Mwanajeshi huyo yupo salama salmini,” Rais Trump alisema katika ujumbe huo.
Wanajeshi wawili waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya kivita walijiondoa kutoka kwa ndege hiyo punde tu hali ya hatari ilipojitokeza. Rubani mmoja aliokolewa Ijumaa na wanajeshi wenzake wa Marekani.
Mamlaka za Iran zimesema kwamba ndege hiyo ya kivita ilidunguliwa na mfumo wake wa makombora ya kutoka ardhini kuelekezwa angani.
Taarifa za ziada kuhusu operesheni ya uokoaji na jinsi ilivyotekelezwa bado zinaendelea kutolewa.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment