
Mhandisi Kambarage Masato Wasira
Na Mwabdishi Wetu
Dar es Salaam
---------------------
Mhandisi Kambarage Masato Wasira, mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Tanzania Bara, Stephen Wasira, ni mmoja wa makada wanaume sita wa chama hicho walioteuliwa kuwania nafasi mbili katika Bunge la Afrika Mashariki.
Makada wengine walioteuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana, ni Stephen Lujwahuka Byabato, Cosato David Chumi, Jabir Jafar Bwanika, Paschal Lawrence Masalu na Suleiman Hassan Serera.
Aidha, Kamati Kuu hiyo iliwateuwa wanawake watatu - Chikulupi Njelu Kasaka, Fatuma Abdallah Kange na Jesca Julias Mshama kuwania nafasi moja katika Bunge la Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na CCM, wateule hao watapigiwa kura za maoni katika kikao cha wabunge wote wa chama hicho tawala, kitakachofanyika jijini Dodoma leo Aprili 30, 2026 saa saba mchana.
No comments:
Post a Comment