
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, akiwemo Mhandisi Peter Philip Mwasalyanda aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, ilieleza kwamba Mhandisi Mwasalyanda anachukua nafasi ya Dkt. Jabiri Kuwe Bakari ambaye amemaliza muda wake.
Rais Samia pia amemteua Dkt. Jabiri Kuwe Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), ambapo anachukua nafasi ya Salim Ramadhani Msangi ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Naye Angela Charles Kizigha ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais kuhusu Masuala ya Jamii.
Wakati huo huo, Rais Samia amempangia Balozi Mobhare Holmes Matinyi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Algeria, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment