NEWS

Friday, 24 April 2026

ZAMCOM wakutana Tanzania kujadili maji ya kimataifa




Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
--------------------

Maji ya kimataifa ni moja ya rasilimali inayoleta amani katika nchi mbalimbali zinazonufaika na wananchi wake.

Akifungua kikao cha 13 cha Baraza la Mawaziri la Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (ZAMCOM) jijini Dar es salaam jana, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alisema maji hayana mpaka na yanakusanya watu kwa maendeleo yao.

Waziri Aweso ambaye katika mkutano huo ni Mwenyekiti aliainisha kuwa umoja wa wananchi na nchi walizopo umeletwa na maji ya kimataifa yanayovuka mipaka ya nchi zao.

Al;isema ni muhimu kuwa na rasilimali za kutosha ili kuleta maendeleo na wananchi wanashirikishwa kutunza rasilimali za maji ili kuleta maendeleo katika sekta nyingine za uchumi.

Alisisitiza kwa wajumbe wa mkutano huo kuwa maji ni muhimu na yanahitajika kuleta maendeleo kwa wananchi.

ZAMCOM inagusa maisha ya wananchi zaidi ya milioni 51 na imekusanya nchi za Tanzania, Angola, Zambia, Malawi, Namibia, Botswana, Zimbabwe, na Msumbiji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages