
Na Mwandishi Wetu
Serengeti
----------------
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, amempogeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, akisema ni kiongozi wa kipekee mwenye unyenyekevu wa hali ya juu.
Jaji Mkuu aliyasema hayo jana katika harambee kubwa iliyoandaliwa na Nyansaho Foundation kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa miradi hiyo katika Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Musati Central, wilayani Serengeti, Mara.

Jaji Mkuu Masaju (kulia mbele) na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega (kushoto), wakitoka kuzindua kanisa hilo kabla ya kushiriki harambee ya ujenzi wa zahanati na shule. Aliyevaa shati jeupe ni Waziri Nyansaho.
Kiasi cha shiingi zaidi ya bilioni 1.4 kilichangwa na wadau mbalimbali katika harambee hiyo ambayo iliongozwa na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega.
Harambee hiyo ilitanguliwa na uzinduzi wa Kanisa la SDA Musati Central ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Nyansaho Foundation kwa gharama ya shilingi milioni 500.

Tukio la ukataji wa utepe kuashiria uzinduzi wa Kanisa la SDA Musati Central
“Dkt. Rhimo Nyansaho ni mnyenyekevu, jambo hili nibkubwa, wengi wetu Mungu akitubariki tunakuwa na kiburi,” Jaji Mkuu Masaju alisema.
Dkt. Nyansaho ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Nyansaho Foundation ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya kijamii katika mkoa wa Mara katika miaka ya hivi karibuni.

Mtoto wa Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere (katikati), akisalimiana na Waziri Nyansaho (kulia) na Waziri Ulega katika harambee hiyo.
Kw upande wake, Waziri Ulega alimuelezea Dkt. Nyansaho kama kiongozi wa mfano, akitolea mfano jinsi tukio hilo lilipata mwitikio mkubwa wa wakazi na viongozi wa mkoa wa Mara wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Kanali Evans Mtambi.
“Wana-Mara hongereni sana kwa kuwa na Dkt. Rhimo Nyansaho. Kwa kweli kazi anazozifanya ni kubwa na za mfano wa kuigwa,” alisema Waziri Ulega ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na idadi kubwa ya wambunge wa mkoa huo.

Aidha, Waziri Ulega alisema kazi anazofanya Dkt. Nyansaho kupita taasisi yake - Nyansaho Foundation zinaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za jamii kwa wananchi.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, alisema Taasisi ya Nyansaho imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mkoa huo.
“Tunampongeza sana Dkt. Nyansaho kwa kazi nzuri, shule zetu zote za sekondari zimepata mabati kutoka Nyansaho Foundation,” alisema Chandi.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, akifuatilia jambo katika harambee hiyo ambapo yeye alichangia shilingi milioni 10.
Awali, Waziri Dkt. Nyansaho alisema fedha zilizopatikana katika harambee hiyo zitajenga zahanati na shule kwa manufaa ya wakazi wote wa Musati na vijiji jirani.
“Siku ya leo sisi tumefurahi sana kwa shughuli hii kuisha salama [ujenzi wa Kanisa la SDA MUsati Central], hekalu la Mungu limekamilika,” alisema Dkt. Nyansaho.
![]() |
| (Picha zote na Mara Online News) |
Mwenyekiti huyo wa Nyansaho Foundation aliongeza: “Tukiwa na zahanati itahudumia watu wote na lengo letu pia tujenge shule kuanzia ‘nursery’ hadi kidato cha sita.”
Kwa upande wao, vongozi wa Kanisa la SDA walishukuru Taasisi ya Nyansaho kwa kuwajengea kanisa la kisasa na changizo hilo la ujenzi zahanati na shule.
“Kanisa hili limefanya watu wengi kufahamu eneo la Musati, leo tumezindua kanisa zuri na nyumba ya mtumishi. Hii ni zawadi ambayo haitasahaulika,” alisema mmoja wa viongozi wa SDA katika hafla hiyo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Majeshi, Jacob Nkunda, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Mara, Christopher Mwita Gacuma na Askofu wa Kanisa la SDA Jimbo la North Mara, miongoni mwa wengine.

No comments:
Post a Comment