NEWS

Tuesday, 21 April 2026

Tume ya Uchunguzi matukio ya Oktoba 29 kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Samia kesho



Jaji Othman Chande

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
---------------------

Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kesho Aprili 23, 2026.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande, aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Aprili 22, 2026.

Jaji Chande alisema ripoti hiyo itakuwa msingi muhimu wa kutoa mwelekeo kuhusu matukio hayo.

Alibainisha kuwa watu 63,603 wameifikia tume hiyo kutoa ushahidi wao kwa njia mbalimbali, ikiwemo kukutana ana kwa ana, kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na dodoso.

Alifafanua kuwa kazi ya tume hiyo ilihusisha ukusanyaji wa ushahidi, maoni ya wadau mbalimbali na uchambuzi wa kina wa taarifa zilizokusanywa.

Tume hiyo ilizinduliwa Rais Samia, Novemba 20, 2025.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages