NEWS

Thursday, 23 April 2026

Ripoti ya Uchunguzi ya Jaji Chande yasema watu 518 walikufa katika vurugu wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025



Jaji Mohamed Chande Othman, akiwasilisha ripoti ya tume hiyo kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
--------------------

Hatimaye ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025 imewekwa hadharani.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mohamed Chande Othman (Jaji Mkuu Mstaafu), amesoma na kuwasilisha ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, jijini Dar es Salaam leo Aprili 23, 2026.

Jaji Chande amesema uchunguzi wa tume hiyo umebaini kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha katika vurugu hizo ni 518, wakiwemo wanaume 490 na wanawake 28.

Amefafanua kuwa mkoa wa Dar es Salaam uliongoza kwa kuwa na watu 182 waliofariki dunia ukilinganisha na mikoa ya Mwanza, Mbeya na Arusha.

Jaji Chande ameeleza kwamba watu 373 walipoteza maisha kabla ya kufkishwa hospitalini.

Akizungumza mara baada ya kupokea ripoti hiyo ya Tume ya Uchunguzi, Rais Samia ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa haraka iwezekanavyo.

Kazi ya Tume hiyo ya Uchunguzi ambayo iliundwa na baadaye kuzinduliwa Rais Samia, Novemba 20, 2025, ilihusisha ukusanyaji wa ushahidi, maoni ya wadau mbalimbali na uchambuzi wa kina wa taarifa zilizokusanywa.

Hafla hiyo ya kusoma na kuwasilisha kwa Rais Samia ripoti hiyo ya Tume ya Uchunguzi, imehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini na mabolozi wa mataifa mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages