NEWS

Friday, 15 May 2026

Mfanyabiashara Mtanzania Nyambari Nyangwine atoa msaada wa vitabu vya Kiswahili nchini Rwanda



Sehemu ya wanafunzi na walimu wa Shule ya St. Marie Riene ya nchini Rwanda wakifurahia msaada wa vitabu uliotolewa na mfanyabiashara Mtanzania, Nyambari Nyangwine, leo.

Na Mwandishi Wetu

Mfanyabiashara Mtanzania, Nyambari Nyangwine, ameipatia Shule ya Sekondari St. Marie Riene ya nchini Rwanda msaada wa vitabu mbalimbali vya Kiswahili.

“Leo asubuhi nimefurahi kutoa msaada wa vitabu vya Kiswahili katika shule moja ya private (binafsi) nchini Rwanda,” Nyangwine amewambia waandishi wa habari muda mfupi baada ya wasaidizi wake kukabidhi vitabu hivyo kwa niaba yake.
Mwakilishi wa Nyambari Nyangwine (kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu kwa Mkurugenzi wa Shule ya St. Marie Riene, mapema leo asubuhi.

Nyangwine ambaye pia ni mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini Tanzania, amesema vitabu hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita.

“Vitabu hivi vitasaidia kukuza lugha ya Kiswahii kwa majirani zetu wa Rwanda,” amesema Nyangwine ambaye pia ni mwanasiasa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime kwa tiketi ya chama tawala - CCM.

Nyambari Nyangwine

Nyangwine pia amekuwa akitoa misaada ya vitabu vya kiada na ziada katika maeneo mbalimbali Tanzania kupitia tasisi yake - Nyambari Nyangwine Foundation, ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za serikali katika kuinua taaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages