
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na Mwandishi Wetu
---------------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia ameunda Tume hiyo kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Hivyo, Rais Samia amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Shabani Ally Lila, kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Aidha, kiongozi huyo wa nchi amewateua Majaji wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari, kuwa Makamishna wa Tume hiyo.
No comments:
Post a Comment