
Mchungaji Dkt. Benjamini Biha (kushoto) akiwashukuru Simion Kiles Samwel na mke wake, Esther, katika hafla ya uzinduzi wa nyumba ya mchungaji waliyojenga katika Kanisa la SDA Turwa, mjini Tarime.
Tarime
-------------
Familia ya Mr & Mrs Simion Kiles Samwel imejenga na kukabidhi nyumba ya kisasa ya mchungaji katika Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Turwa lililopo Tarime mjini, mkoani Mara.
Nyumba hiyo ilizinduliwa na Mwenyekiti wa Kanisa la SDA Jimbo la North Mara Field, Mchungaji Dkt. Benjamin Biha, jana Jumamosi.
Uzinduzi huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo, akiwemo Mwenyekiti wa Jimbo la Mara, Mchungaji John Matongo.
Viongozi hao wa kirogo walimshukuru Kiles na mke wake, Esther, kwa zawadi hiyo ya nyumba ya mchungaji wa kanisa hilo na kuwaombea baraka zaidi.

Kiles na mke wake, Esther (kushoto), wakimkabidhi Mchungaji Dkt. Biha funguo za nyumba hiyo.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, alifika kanisani hapo na kupata fursa ya kuona kazi nzuri iliyofanywa na familia hiyo ya kujenga nyumba hiyo ya mchungaji.
Katika salamu zake, Meja Gowele aliwaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuhimiza amani kwa ustawi na maendeleo ya taifa la Tanzania.
(Picha zote na Sauti ya Mara)
No comments:
Post a Comment