
Waziri Mkuu Mwigulu akipanda ndege kuondoka jijini Dar es Salaam leo Mei 10, 2026 kuelekea Nairobi kumwakilisha Rais Samia kwenye Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa.
---------------------------
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 10, 2026 ameondoka nchini kuelekea Nairobi, Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa (Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and Growth Summit).
Mkutano huo utafanyika Mei 11–12, 2026, lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa katika sekta mbalimbali, ikiwemo biashara, teknolojia, nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu na viwanda.
Aidha, mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unalenga pia kukuza uwekezaji mpya kati ya Afrika na kampuni za Ufaransa, kujenga ushirikiano unaotajwa wa usawa na kujadili mageuzi ya mfumo wa fedha na maendeleo endelevu ya Afrika.
Mkutano huo unawakutanisha wadau wa maendeleo, wawekezaji na sekta binafsi, na umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Samoei Ruto na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, Emmanuel Macron.
No comments:
Post a Comment