![]() |
| Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake, Rais Vladimir Putin nchini Urusi |
Ziara ya kihistoria ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi iliyomalizika mwishoni mwa wiki italeta neema ya kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali za kiuchumi nchini.
Hii ni kwa mujibu wa mawaziri waliombatana na Rais Samia katika ziara hiyo ya siku tatu iliyofanyika kuanzia Juni 3 hadi 5 mwaka huu.
Mawaziri hao, Mahmoud Thabiti Kombo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Prof Kitila Mkumbo wa Ofisi ya Rais Mipango, waliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kuwa, kwa ujumla, ziara imeimarisha zaidi ari ya diplomasia ya ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
Prof Mkumbo alisema sekta tisa muhimu zitakazonufaika na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ni kilimo, nishati, elimu na mafunzo, madini, viwanda, usafiri na usafirishaji, utalii, uchumi wa kidijitali pamoja na biashara na uwekezaji.
Alisema Kituo Maalum cha Uwekezaji Tanzania (TISEZA) kimefanikiwa kuwavutia wawekezaji katika sekta za madini, utalii, kilimo, uzalishaji dawa, miundombinu, mbolea na sekta ya fedha.
Ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi ni wa muda mrefu taifa hhiili kubwa las Afrika lipate uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1961.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ndiye alikuwa kiongozi wa kwanza kuitembelea Urusi mwaka 1969.

No comments:
Post a Comment