NEWS

Friday, 12 June 2026

Serena Williams aamua kurudi kwenye ulingo wa tenisi



Serena Williams alipokuwa kwenye ubora wake kwa mchezo wa tenisi.

Na Mwandishi Wetu

Serena Williams alirudi tena kwenye ulingo wa mchezo wa tenisi baada ya karibu miaka minne (siku 1,375) ya kuuacha mchezo huo pale alipojinyakulia ushindi uwanja wa Queen's.

Mashabiki jioni ya Jumanne iliyopita waliujaza Uwanja wa Andy Murray kumwangalia mmoja wa mabingwa wa muda wote wa mchezo huo akirudi uwanjani baada ya kutundika daluga zake.

Akicheza pamoja na binti mdogo wa Canada, Victoria Mboko, Serena, (44), hakuonekana ameusahau mchezo huo kwa kuwa wawili hao walishinda 7-6 (7-2) kwa 6-2 dhidi ya wapinzani wao Erin Routliffe na Nicole Melchar- Martinez.

"Ilikuwa ni furaha," alisema Serena baada ya kumalizika kwa mchezo. "Ilikuwa ni furaha kucheza na Victoria. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kuifanya timu yetu ipate ushindi. Nilikuwa namtegemea. Hatujawahi kucheza pamoja lakini ilionekana kama tumezoeana."

Alipoulizwa kwanini alirudi ulingoni, aliongeza: "Sikuwa na kitu kizuri zaidi cha kufanya. Nilichoka kukaa nyumbani. Watoto wangu wako likizo kutoka shuleni wakati wa majira ya joto kwanini nisirudi kwenye mchezo niliyoupenda?"

"Sijawahi kucheza hapa; ni wanaume tu waliokuwa wakicheza. Ni jambo la kufurahisha kucheza mahali maalum kama hapa."

Serena aliachana na mchezo wa tenisi 2022 baada ya kushinda mara 23 kwenye mashindano ya Grand Slam kwa miaka 27 ya kuutumikia mchezo huo.

Shamrashamra za mchezaji huyo kurudi kwenye ulingo wa tenisi zilianza kujitokeza mwaka jana wakati jina lake lilipojitokeza kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa kupimwa kuhusu matumizi ya dawa na kwenye orodha ya Wakala wa Kimataifa wa Tenisi (ITIA).

NI NINI HATIMA YA SERENA NA DADA YAKE VENUS?

Dada yake Serena, Venus William, mwenye umri wa miaka 45, bado anacheza tenisi, jambo linalodhihirisha kuwa umri ni namba tu.

Serena anasema "nitarudi tena kwenye ulingo wa tenisi" kama walivyofanya wanamichezo wengine marafiki zake, Lindsey Vonn na Allyson Felix.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages