NEWS

Thursday, 4 June 2026

Ziara ya kihistoria: Rais Samia atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima Chuo Kikuu cha Rudn Urusi



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Oleg Yastrebov, katika hafla iliyofanyika chuoni hapo jijini Moscow, leo Juni 4, 2026.

Rais Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Udaktari wa Heshima kutokana na mchango wake katika mageuzi ya sekta ya elimu, juhudi zake za kuimarisha diplomasia ya Tanzania na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania kimataifa, ikiwemo kupitia sekta ya utalii.

Akizungumza baada ya kutunukiwa shahada hiyo, Rais Samia amesema heshima hiyo siyo ya mafanikio yake binafsi, bali ni utambuzi wa mchango wa Watanzania wote katika maendeleo ya taifa na ushirikiano wa kimataifa.

"Shahada hii haihusu mafanikio yangu binafsi... Naipokea kwa upole, kama Rais wa Tanzania, mtoto wa Afrika na rafiki wa Russia. Siipokei kwa ajili yangu, bali kwa ajili ya Watanzania," amesisitiza Rais Samia.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages