![]() |
| Kutoka kushoto ni Aggrey Mwanri na Paul Chacha |
Na Mwandishi Wetu
Zanzibar
-------------
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya mabadiliko ya sekretarieti yake kwa kuteua wajumbe wapya wanne kuchukua nafasi za waliowekwa kando.
Uteuzi huo umefanyika leo Jumatano, Julai 29, 2026, katika kikao cha NEC hiyo kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, visiwani Zanzibar.
Katibu wa NEC ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewataja wajumbe wapya kuwa ni aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara kuchukua nafasi ya John Mongella.
Kihongosi amewataja wengine kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora wa sasa, Paul Chacha, ambaye ameteuliwa kuwa Katibu wa Oganaizesheni wa CCM, ambapo anachukua nafasi ya Issa Haji Gavu.\
Wengine ni Abdi Mohamed Abdi ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na Jamal Kassim Ali aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha kuchukua nafasi ya Joshua Mirumbe.

No comments:
Post a Comment