NEWS

Thursday, 9 July 2026

Halmashauri ya Serengeti DC yakusanya bilioni 6.29/- mapato ya ndani



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti jana.

Na Godfrey Marwa
Serengeti
----------------

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imekusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 6.29 sawa na asilimia 86 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 7.275 katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Hayo yalielezwa jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo cha kilichojadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambacho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.

Sehemu ya madiwani kikaoni

Akizungumza katika kikao hicho, Kanali Mtambi alilitaka baraza hilo kusimamia kwa karibu ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo ili iweze kufikia lengo lake katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Kwa upande mwingine, Kanali Mtambi aliahidi kuisaidia halmashauri hiyo kufanikisha juhudi za kurejeshewa haki yake ya mapato yatokanayo na shughuli za utalii yanayoelekezwa katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti inapakana na Hifadhi ya Taifa Serengeti ambayo eneo lake kubwa liko ndani ya halmashauri hiyo ya mkoani Mara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages