NEWS

Thursday, 9 July 2026

RC Mtambi aihamasisha Butiama DC kuendeleza rekodi ya hati safi



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama jana.

Na Godfrey Marwa
Butiama
---------------

Mkuu wa Mkoa (RC) ya Mara, Kanali Evans Mtambi, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kwa kupata Hati Safi kwa miaka mitano mfululizo na kuitaka kuendeleza rekodi hiyo.

Kanali Mtambi alitoa pongezi hizo jana wakati akizungumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo lililojadili taarifa ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2024/2025.

"Nawapongeza halmashauri kwa kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo, huo ni ushahidi kuwa kazi inafanyika, tuhakikishe tunaendeleza wimbi la kuwa na hati safi,” alisema.

Sehemu ya madiwani mkutanoni

Pia, Kanali Mtambi aliipongeza halmashauri hiyo kwa kuvuka lengo la makusanyo ya mapato ya ndani katika kipindi hicho na kuitaka kutafuta vyanzo vipya vya mapato hayo.

Aidha, aliitaka halmashauri hiyo kuhamasisha na kutoa elimu kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa za mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Naye mbunge wa Jimbo la Butiama, Dkt. Charles Mahera, mlisisitiza umuhimu wa madiwani na watendaji kuendelea kushirikiana katika kuisimamia halmashauri hiyo ili kuongeza kasi ya utekeleza wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages