
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.
Musoma
---------------
Mwenge wa Uhuru 2026 unatarajiwa kuanza mbio zake mkoani Mara kesho Jumamosi, Agosti 1, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amesema.
Kwa mujibu wa Mtambi, Mwenge utatembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 63 yenye thamani ya shilingi bilioni 174 katika halmashauri zote tisa za mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa amesema hayo mapema leo asubuhi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Musoma kuhusu maandalizi ya kupokea Mwenge huo.
Amefafanua kuwa Mwenge utapokewa kesho saa 12 asubuhi katika uwanja wa Shule ya Msingi Balili na kuanza mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kanali Mtambi ametoa wito kwa wananchi wa Mara kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru na kushiriki katika matukio yaliopangwa kufanyika katika mkoa huo.
Kauli ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 ni “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo”.
No comments:
Post a Comment