NEWS

Thursday, 24 September 2026

Ndejembi ashiriki Mkutano wa Africa CDC nchini Marekani




Na Mwandishi Wetu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi (pichani katikati), leo Alhamisi, Septemba 24, 2026 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Viongozi kuhusu afya ya Mama na Mtoto.

Mkutano huo ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81) jijini New York, Marekani.

Pia, Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, Dkt. Jean Kaseya na mwenza wa Rais wa Benin, Nathalie Vilette Wadagni.

Washiriki wengine ni wadau wa maendeleo wakiwemo, Gates Foundation, Global Fund, Gavi, UNFPA, Unicef, Suzan Thompson Buffett Foundation, Beginning Fund na viongozi kutoka Umoja wa Afrika (AU).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages