
Deogratius John Ndejembi
Na Mwandshi Wetu
Jina la Deogratius John Ndejembi litawasilishwa Bungeni kwa uthibitisho wa kuwa Makamu wa Rais mpya baada ya jana Alhamisi kupendekezwa na kikao maalum cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Ndejembi, 43, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nishati, anamrithi Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyejiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais juzi Jumanne, Agosti 25, 2026.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, Dkt. Nchimbi amefukuzwa uanachama kwa kile kilichodaiwa kukiuka maadili na kanuni za chama hicho tawala.

Dkt. Emmanuel Nchimbi
Kufukuzwa kwa kiongozi huyo mzoefu wa siasa za Tanzania ni moja ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM iliyoketi chini ya Mwenyekiti wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya Dkt. Nchimbi kumwandikia Rais barua ya kujiuzulu.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatazamiwa kumthibitisha Ndejembi kwa kauli moja kama ilivyopendekezwa na Kamati Kuu ya CCM ili achukue nafasi ya mtangulizi wake, Dkt. Nchimbi.
Kiutaratibu, Ndejembi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, itabidi aachie kiti hicho kupisha kuchaguliwa kwa mwakilishi mwingine wa wananchi.
Inatazamiwa kwamba baada ya kuthibitishwa na Bunge, Makamu wa Rais mpya atachukua nafasi yake rasmi Septemba 9, 2026 baada ya kuapishwa na Rais.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya nwaka 1977, Makamu wa Rais ni msaidizi mkuu wa Rais katika ngazi ya utawala wa nchi.
No comments:
Post a Comment