NEWS

Sunday, 16 August 2026

TAWIRI yaagizwa kutatua kero ya tembo wanaoendelea kutesa wananchi



Tembo wakiharibu mazao shambani

Na Mwandishi Wetu,
Dodoma
---------------

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imetakiwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la wanyamapori wakali na waharibifu, wakiwemo tembo kwa ustawi wa wananchi wanaoishi kandokando ya hifadhi za taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema serikali inapenda kuona wananchi walioko kandokando ya maeneo yaliyohifadhiwa wanakuwa na maisha endelevu bila kero za wanyama hao.

Waziri Kijaji aliyasema hayo jijini Dodoma hivi karibuni, wakati wa kujadili taarifa ya utendaji wa TAWIRI kuhusu mafanikio na changamoto za utendaji.

Alisema ni muhimu TAWIRI kuishauri serikali katika masuala yote ya sayansi ya wanyamapori. "Njooni na suluhu ya kudumu kuhakikisha ustawi wa wananchi kwenye hifadhi za taifa,” alisema.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na migogoro kati ya wanyamapori na binadamu - inayohusu uharibifu wa mazao na kushambulia watu.

Wakati mwingine serikali imekuwa ikilazimika kuwalipa fidia wananchi walioharibiwa mali zao na wanyamapori waharibifu, hasa tembo wanaovamia na kuharibu mashamba ya mazao vijijini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages