NEWS

Sunday, 2 August 2026

Wanakijiji Musoma Vijijini kukamilisha ujenzi Sekondari ya Ufundi Mwigombe



Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo.

Na Mwandishi Wetu
Musoma
--------------

Wakazi wa kijiji cha Kiriba katika jimbo la Musoma Viijini, Mara wamedhamiria kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mwigombe kabla ya kufunguliwa Januari 2027.

Viongozi wa serikali wamepanga Mwenge wa Uhuru uiwekee shule hiyo jiwe la msingi Agosti 8, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini juzi, ujenzi wa shule hiyo unawashirikisha wanavijijji, familia ya Mashenene, wazaliwa wa kata ya Kiriba, Mbunge Prof. Sospeter Muhongo na wadau wa maendeleo, zikiwemo benki za CRDB na NMB.

Sehemu ya wanakijiji wakiendelea na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mwigombe

Taarifa hiyo ilisema mbunge huyo atawafanyia wanakijiji wa Kiriba sherehe kuwapongeza kwa juhudi za kujitolea kuchangia maendeleo kwa kushirikiana na serikali.

Mafanikio yatakayowakusanya wanakijiji pamoja ni ujenzi wa Sekondari ya Ufundi Mwigombe na ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kiriba.

Wananchi na viongozi wa jimbo la Musoma wanaendelea kuishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugharimia miradi ya maendeleo katika jimbo hilo.

Musoma Vijijini ni moja ya majimbo kadhaa mkoani Mara ambayo yamepiga hatua kubwa katika kuimarisha sekta ya elimu na nyingine za kijamii na kiuchumi.

Viongozi wa jimbo wakiongozwa na Mbunge Muhongo wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushirikiana katika kujiletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages