
Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Massana Mwishawa, akizungumza jijini Dodoma leo Jumatano katika kikao cha maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na El Niño.
Dodoma
---------------
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo Septemba 16, 2026 limeshiriki kikao cha wadau cha maandalizi ya kukabiliana na athari za majanga yanayoweza kutokea kwa kusababishwa na mvua za El Niño, kilichofanyika jijini Dodoma.

Kikao hicho ambacho kimejadili hatua za kuzuia, kujiandaa, kukabiliana na kurejesha hali ya kawaida kabla, wakati na baada ya athari za El Niño.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Benard Marcelline, ameongoza kikao hicho ambapo amesisitiza umuhimu wa taasisi na wadau wa utalii kuwa na mipango madhubuti ya tahadhari.
Marcelline ametaja mipango hiyo kuwa ni pamoja na kutambua maeneo hatarishi, kuimarisha miundombinu, kuandaa rasilimali, kuelimisha umma na kuimarisha mifumo ya mawasiliano na huduma za dharura.
No comments:
Post a Comment