NEWS

Sunday, 4 October 2026

Tahadhari ya El Nino: Kamishna wa Uhifadhi TANAPA aelekeza uimarishaji miundombinu Hifadhi ya Saanane



Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Massana Mwishawa (katikati), akielekeza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño, wakati wa ziara yake katika hifadhi hiyo jijini Mwanza jana.

Na Philipo Hassan
Mwanza
-------------

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Massana Mwishawa, ameelekeza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño, ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho na ukarabati wa miundombinu muhimu inayotumiwa na watalii.

Kamishna Mwishawa aliyasema hayo jana Jumamosi alipofanya kikao na Maafisa na Askari Uhifadhi wa hifadhi hiyo jijini Mwanza, ambapo alielekeza ukarabati maboresho na ukarabati huo vifanyike sambamba na kuongeza urefu wa ukingo wa uzio katika maeneo ya watalii kupanda boti kwenda hiofadhini.

Pia, kufanya ukarabati wa boti na miundombinu mingine muhimu ili kuimarisha uhimilivu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane wakati wa mvua hizo.

Aidha, Kamishna Mwishawa alisisitiza kuongeza bidii katika kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana katika hifadhi hiyo ili kutimiza lengo la serikali la kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii.

Kwa upande wake, Afisa Uhifadhi Mkuu na Kaimu Mkuu wa Hifadhiy a Taifa Kisiwa cha Saanane, Upendo Massawe, alisema hifadhi hiyo inaendelea kusimamia kwa ufanisi shughuli za uhifadhi na utalii, ikiwemo kuimarisha ulinzi na usalama wa maliasili, shughuli za ikolojia na mahusiano kati ya hifadhi na jamii.

Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane imeendelea kuvutia watalii wengi wa ndani kutokana na kuwa na mazao mbalimbali ya utalii, ikiwemo utalii wa picha, kutazama wanyama, utalii wa boti, uvuvi wa kitalii, kupiga kambi, matembezi na kula chakula cha hifadhini (Bush lunch).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages