NEWS

Sunday, 21 July 2024

Balozi Mbarouk amwandikia Spika barua ya kujiuzulu ubunge



Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk
---------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
---------------------------

Mbunge wa kuteuliwa na Rais, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amemwandikia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Spika Dkt Tulia Ackson barua ya kujiuzulu ubunge.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge leo Julai 21, 2024, imesema Mbarouk amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kijamii zinazomkabili.

“Ninalazimika kuchukua uamuzi wa kujiuzulu ili nipate nafasi ya kushughulikia changamoto hizo,” taarifa hiyo imemnukuu Balozi Mbarouk.

Kujiuzulu ubunge kwa Balozi Mbarouk kutakwenda sambamba na kuachia pia nafasi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages