NEWS

Monday, 22 July 2024

Serikali ya Rais Samia yatangaza nafasi za ajira za walimu 11,000



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
-----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------

Serikali ya Jamburi ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imetangaza nafasi 11,015 za ajira za walimu nchini, zikiwemo 2,851 za walimu daraja la IIIA.

Serikali ilitangaza nafasi hizo za ajira Julai 20, 2024 kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Mikoa wanakohitajika walimu wa daraja la IIIA na idadi yao ikiwa kwenye mabano ni Njombe (62), Mtwara (153), Dodoma (85), Shinyanga (115), Songwe (101), Iringa (56), Manyara (78), Tabora (116), Singida (110), Tanga (113) na Kagera (133).

Katavi (99), Rukwa (76), Simiyu (120), Mara (173), Geita (90), Ruvuma (140), Kigoma (129), Dar es Salaam (19), Pwani (68), Arusha (116), Mwanza (134), Morogoro (129), Kilimanjaro (124), Mbeya (217) na Lindi (95).
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages