NEWS

Tuesday, 30 July 2024

Chandi: Tumejifunza mengi kwa Kinana akiwa Mlezi wa CCM Mkoa wa Mara



Abdulrahman Kinana na Patrick Chandi Marwa
--------------------------------------------------------

Na Mwandishi WETU
-------------------------------

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa amesema wana-CCM mkoani Mara wamejifunza mambo mengi mazuri kutoka kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana wakati akiwa Mlezi wao.

“Kinana alikuwa Mlezi wetu [CCM] wa Mkoa wa Mara, kichama tumejifunza mengi kutoka kwake, na pia tunamuomba asifunge milango pale tutakapohitaji ushauri kutoka kwake, maana alikuwa kiongozi mahiri sana,” amesema Chandi katika mazungumzo na Mara Online News kwa njia ya simu leo asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa jana Julai 29, 2024 na Katibu wa NEC - Itikati, Uenezi na Mafunzo, Amos Makala, Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia aliridhia ombi la Kinana la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara ambaye alimwandikia barua ya kuomba kupumzika utumishi wa chama hicho.

Katika kumjibu Kinana, Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia alisema “Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako.”

Aidha, Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alimshukuru Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa chama hicho  tawala, na kusema kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa yake kila vitakapohitajika.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages