NEWS

Wednesday, 24 July 2024

Nyambari akutana na Spika wa Bunge la Tanzania Jijini New Delhi



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson (wa tatu kushoto) na Nyambari Nyangwine (wa pili kulia) wakiwa na wenyeji wao walipokutana Jijini New Delhi, India leo.
--------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------

Mfanyabiashara na mchapishaji wa vitabu, Nyambari Nyangwine amekutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson katika Jiji la New Delhi nchini India.

Nyambari na Dkt Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamekutana Jijini New Delhi leo Julai 24, 2024.

Nyambari ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara kupitia chama tawala - CCM, yupo nchini India tangu Jumamosi iliyopita kwa ziara ya siku nane ya kibiashara.

Akizungumza na Mara Online News kwa njia ya simu baada ya kuwasili India, Nyambari alisema alikuwa na ratiba ya kutembelea viwanda vya uchapaji vitabu katika mji wa Mumbai.

Pia, viwanda vya korosho na nguo katika mji wa Gujarat, kiwanda cha karatasi katika mji wa Kolkata na Ubalozi wa Tanzania nchini India katika Jiji la New Delhi.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages