
Mwenyekiti wa UWT CCM Mkoa wa Mara, Nancy Msafiri akizungumza na wanachama wa jumuiya hiyo wilayani Tarime jana.
-------------------------------------------------
--------------------------------------
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara imeahidi kuwasaidia wanachama wake watakaojitokeza kugombea uongozi katika chaguzi zijazo.
“Sehemu yoyote atakayosimama mwanamke, timu ya mkoa tumejipanga kumsaidia,” alisema Mwenyekiti wa UWT CCM Mkoa wa Mara, Nancy Msafiri wakati akizungumza na wanachama wa jumuiya hiyo wilayani Tarime jana Julai 22, 2024.
Nancy alisisitiza katika mkutano uliofanyika jimbo la Tarime Vijijini na baadaye jimbo la Tarime Mjini kwamba uongozi wa UWT Mkoa utaungana na timu ya wilaya kuwanadi wanachama wake kwa wananchi.

Wajumbe wakifuatilia hotuba
ya kiongozi kikaoni.
--------------------------------------------------
“Lakini pia tutaungana na wabunge pamoja na madiwani, anaposimama mwanamke lazima tusimame, ndio maana tuna kaulimbiu inayosema ‘mshike mkono mwenzio’, wakati ni sasa.
“Tunataka na wewe mwanamke uje ushike kiti cha udiwani tena wa kata, uje ushike nafasi ya kijiji, mtaa, kitongoji, ushike hata ubunge wa jimbo.
“UWT tuko tayari kuhakikisha jumuiya inaendelea kuwa imara mbele ya Chatanda na Shomari, mbele ya jemedari wetu Mama Samia Suluhu Hassan,” alisema Nancy.
Aidha, katika ziara hiyo yakiongozi huyo, wanachama wapya zaidi ya 300 walipokewa na kujiunga na UWT.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT CCM Wilaya ya Tarime, Neema Charles aliwashukuru wanajumuiya kwa kujitokeza kwa wingi katika mikutano iliyohutubiwa na Mwenyeiti wa Mkoa.

---------------------------------------------------
Lengo lilikuwa kuhamasisha wanachama wa UWT kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura na kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika nchini mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwakani.
Katika ziara hiyo, Mwenyekiti Nancy aliambatana na viongozi mbalimbali wa chama akiwemo Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT, Rhobi Samwelly ambaye alitumia nafasi hiyo kuiomba jamii kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia, kiuchumi na kisiasa dhidi ya wanawake.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
- 1.TIC watembelea kahawa ya Tarime inayotamba soko la dunia
- 2. Nyambari akutana na Spika wa Bunge la Tanzania jijini New Delhi
- 3.Rais Samia ang'oa vigogo TTCL, Posta na Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
- 4.Balozi Mbarouk amwandikia Spika barua ya kujiuzulu ubunge
- 5.Maswi, Ridhiwan wang’ara teuzi za Rais Samia, Nape na Makamba wavuliwa uwaziri, Mashinji na Afraha wahamishwa Serengeti
- 6.Biden ajiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais Marekani
No comments:
Post a Comment