NEWS

Friday 9 August 2024

Botswana Yatangaza Mapumziko Maalum kwa Ushindi wa Letsile Tebogo katika Michezo ya Olimpiki.

Mwanariadha wa Botswana ,Letsile Tebogo (mbele) katika mbio alizoibuka mshindi mashindano ya Olimpiki.
        ----------

Rais wa Botswana ametangaza Ijumaa alasiri kuwa sikukuu ya kusherehekea Letsile Tebogo, ambaye siku ya Alhamisi aliandikisha historia ya kuwa Mwafrika wa kwanza kushinda mbio za Olimpiki za mita 200.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 aliwapita wapinzani wake Kenny Bednarek na Noah Lyles mjini Paris kushinda medali ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki ya Botswana katika mchezo wowote.

Tebogo sasa anatambuliwa kama mtu wa tano kwa kasi zaidi katika historia kwa umbali. Ametunuku ushindi wake kwa marehemu mama yake, ambaye aliaga dunia mwezi Mei. 

                                                         CHANZO:BBC

Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages