NEWS

Friday 23 August 2024

Rwanda yapiga 'stop' utendaji wa mashirika 43 ya kidini kwa ukiukaji wa sheria




Serikali ya Rwanda imetangaza orodha ya majina ya mashirika ya kidini yaliyopigwa marufuku kwa kukiuka sheria.

Orodha hiyo inajumuisha mashirika 43 ambayo yamekuwa yakiendesha shughuli zake katika wilaya 18 nchini Rwanda.

Hatua hii imetokana na uchunguzi unaoendelea wa utendaji wa mashirika yenye misingi ya imani ulioanza Julai 28, 2024.

Tangu Julai, Rwanda imefunga makanisa 4,000 katika kipindi cha mwezi kutokana na kushindwa kuzingatia kanuni za afya na usalama.

Hatua hiyo iliathiri zaidi makanisa madogo ya Kipentekoste - ambayo baadhi yaliendesha ibada nje ya mapango, au kwenye kingo za mito.

"Hii haifanywi kuwazuia watu kusali, bali kuhakikisha usalama na utulivu wa waumini," Waziri wa Serikali ya Mitaa, Jean Claude Musabyimana aliviambia vyombo vya habari vya serikali.

Ni msako wa kwanza mkubwa tangu sheria ilipobuniwa miaka mitano iliyopita kudhibiti maeneo ya ibada.

Sheria kuhusu Imani inayataka makanisha kuendesha ibada kwa mpangilio katika mazingira salama na kuharamisha matumizi yao vipaza sauti.

Sheria hiyo pia inawalazimu wahubiri wote kupata mafunzo ya kidini kabla ya kufungua kanisa.

Sheria ilipopitishwa mwaka 2018, takriban makanisa 700 yalifungwa hapo awali.

Wakati huo, Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema nchi hiyo haihitaji nyumba nyingi za ibada, kwa maelezo kuwa idadi hiyo kubwa inafaa tu kwa uchumi ulioendelea zaidi na njia za kuziendeleza.

Mengine ni makubwa, yanavutia maelfu ya waumini kila Jumapili, lakini mengine ni majengo madogo yaliyojengwa bila idhini.
Chanzo: BBC
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages