NEWS

Thursday, 24 October 2024

Mwenyekiti CCM Mara awapongeza wanachama kwa uchaguzi wa amani



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa.
---------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa ametuma salamu za kuwapongeza na kuwashukuru wanachama wa chama hicho tawala kwa kufanya uchaguzi wa ndani [kura za maoni] kwa amani na utulivu.

“Sasa kazi iliyobaki ni moja - ya kuhakikisha tunashinda uchaguzi wa wa viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji ili CCM iendelee kushika dola na kuunda Serikali,” amesema Mwenyekiti Chandi katika mazungumzo na Mara Online News kwa njia ya simu leo Oktoba 23, 2024.

Uchaguzi wa kuwapata wagombea kupitia kura za maoni ndani ya chama hicho tawala ulifanyika jana kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote Novemba 27, 2024.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages