
Mwandishi Wetu, Magu



Shirika lisilo la Serikali la Mwanza Youth and Children (MYCN) limewataka vijana wanufaika wa elimu ya utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kuwa mabalozi wazuri wa utunzaji wa mazingira.
Mratibu Miradi wa shirika hilo, Ester Kusekwa aliyasema hayo wakati wa kongamano la vijana zaidi ya 500 la elimu ya utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lililofanyika Kisesa wilayani Magu, Mwanza hivi karibuni.


Kusekwa alisema ili dunia iendelee kuwa salama, ni lazima kila mwanajamii ahakikishe anatunza mazingira vizuri kwa kufanya usafi katika eneo lake na kupanda miti ya kutosha.
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika kongamano hilo la vijana, ni fursa za kiuchimi kwa vijana pamoja na uzalendo.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mzava aliwataka viongozi wilayani Magu kuongeza makongamo ili kuwezesha vijana kupata elimu kwa kina.
No comments:
Post a Comment