Na mwandishi wetu,Mwanza
Wakati Jiji la Mwanza likizidi kukua ukubwa wake unachangiwa na uwepo wa vitega uchumi mbalimbali sambamba na utalii wa mikutano ya kitaifa na kimataifa.
Miongoni mwa vitega uchumi hivyo ni mradi wa Rock City Malls wenye jengo maarufu kwa shughuli mbalimbali za mikutano, biashara na vitega uchumi anuai.
Chini ya uwekezaji wa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Rock City Malls imeweza kuvutia wapangaji kwa zaidi ya asilimia 90 hadi sasa na thamani yake ikikua hadi kufikia zaidi ya shilingi 100 bilioni.
Meneja wa Rock City Malls Annette Shoo anasema maombi ya kupanga kwenye jengo hilo yanazidi kuongezeka na anatoa ushauri kwa PSSSF kufikiria kuwekeza zaidi kwenye hoteli za hadhi ya nyota 3 na nyota 5 ili kuhudumia wageni wanaofurika kila siku kwa shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano.
Rock City Malls ilianzishwa miaka 5 iliyopita na zaidi ya watu 10,000 hutembelea jengo hilo kila siku.
No comments:
Post a Comment