NEWS

Tuesday 1 October 2024

Waziri Simbachawene aanza ziara ya kikazi mkoani Mara



Waziri George Simbachawene

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, leo ameanza ziara ya siku nne mkoani Mara kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Waziri Simbachawene pia anatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali, kuiwekea mawe ya msingi na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Waziri huyo ameanza ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Musoma Vijjini akiwa ameambatana na viongozi wa mkoa.

Mkoa wa Mara umepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara.

Ziara ya Waziri Simbachawene inatazamiwa kuwa kichocheo cha kukamilika kwa miradi inayoendelea kutekelezwa ili ianze kuhudumia wananchi.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages