
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Mgodi wa North Mara, Michael Kahela (katikati) akipokea tuzo ya Mwajiri Bora.
--------------------------------------
Mgodi wa North North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals, kwa mara nyingine baada ya ushindi wa mwaka jana, umeshinda tena tuzo kubwa ya jumla ya mwajiri bora inayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
Tuzo nyingine ambazo mgodi huo umeshinda ni uwajibikaji kwa jamii, afya na usalama mahali pa kazi, Mshindi wa pili katika kipengele cha Mwajiri Bora sekta binafsi, na uzingatiaji wa kanuni za maudhui ya ndani.
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu nao umeshinda katika kipengele cha uzingatiaji wa sheria na kanuni kutoka mamlaka za usimamizi.
Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko.

Naibu Waziri Mkuu Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko (wa tatu kutoka kushoto) akitoa pongezi kwa Meneja Uhusiano wa Barrick, Georgia Mutagahywa kwa ushindi huo wa mgodi wa North Mara baada ya kumkabidhi cheti.
-------------------------------------
Akizungumzia mafanikio haya ya mgodi wa North Mara, Meneja Uhusiano wa Barrick, Georgia Mutagahywa alisema ushindi wa tuzo hizo unadhihirisha jinsi mgodi huo unavyoendeshwa kwa weledi na viwango vya kimataifa, ukilipa kipaumbele kikubwa suala la uzingatiaji afya na usalama, sambamba na ukuzaji wa vipaji vya Watanzania.
Migodi yote ya Barrick inaongozwa na Watanzania kwani asilimia 96 ya wafanyakazi ni wazawa. Pia kampuni imekuwa na mpango wa kuwezesha wafanyakazi wanawake ambapo kwa sasa wanafanya kazi kwa ufanisi katika vitengo mbalimbali.

Wafanyakazi wa Barrick wakisherekea
tuzo za ushindi huo.
-----------------------------------
“Suala la kudumisha uhusiano mzuri na wafanyakazi linapewa umuhimu mkubwa sambamba na kuendesha programu za kuwajengea afya njema kwa kushiriki mazoezi na michezo mbalimbali,” alisema Mutagahywa.
Migodi ya Barrick na Twiga pia imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali kutekeleza miradi ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii za maeneo yanayozunguka migodi yake, hususan katika sekta za elimu, afya, maji safi na salama, na ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Kati ya mwaka 2020 hadi 2024, Barrick North Mara imewekeza shilingi zaidi ya bilioni 22 katika kutekeleza miradi 253 ya kijamii.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Askofu Msonganzila amshukuru Nyambari Nyangwine kuhudhuria Jubilei ya Miaka 40 ya Upadre wake
>>CCM Musoma Vijijini yashinda kwa kishindo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
>>CHADEMA yashinda vijiji 4 Tarime Vijijini katika kata 3, imo Ganyange
>>Miili ya watu 8 waliosombwa na mafuriko mto Mori kuzikwa kesho Tarime
No comments:
Post a Comment