
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Chama kikuu cha upinzani nchini - CHADEMA, kimeambulia uongozi wa Serikali za Mitaa katika vijiji vinne kati ya 88 vilivyopo jimbo la Tarime Vijijini, mkoani Mara.
Vijiji hivyo vinne na kata zake zikiwa kwenye mabano ni Nyakirima (Ganyange), Nyabisaga (Pemba), Soroneta na Kemakorere (Nyarero), ambavyo wagombea wa CHADEMA wameshinda nafasi ya uenyekiti.
“Ni vijiji vinne kati ya vijiji vyote 88 ndivyo CHADEMA wameshinda katika kata za Pemba, Nyarero na Ganyange,” chanzo cha habari cha uhakika kimeiambia Mara Online News mapema leo Ijumaa asubuhi.
Jana, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa alitangaza matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini uliofanyika juzi Novemba 27, 2024 ambao unaonesha kuwa chama tawala - CCM kimepata ushindi wa takriban asilimia 99.
No comments:
Post a Comment