NEWS

Wednesday, 27 November 2024

Miili ya watu 8 waliosombwa na mafuriko mto Mori kuzikwa kesho Tarime



Sehemu ya mto Mori katika mtaa 
wa Bugosi, Tarime mkoani Mara.

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Miili ya watu wanane wa familia moja waliofariki dunia baada ya makazi yao kuvamiwa na kusombwa na mafuriko ya mto Mori katika mtaa wa Bugosi uliopo kata ya Nyamisangura, Tarime mkoani Mara itaagwa na kuzikwa kesho Novemba 28, 2024.

Mafuriko hayo ya mto Mori, unaotiririsha maji kwenda Ziwa Victoria nchini Tanzania, yalitokea Novemba 24, 2024 saa nne usiku.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Mwalimu Saul Mwaisenye, miili hiyo itaagwa kwenye viwanja vya Bugosi, kisha kusafirishwa kwenda kuzikwa katika makaburi ya Magena, nje kidogo ya mji wa Tarime.

Kati ya watu 11 wa familia ya Elias Ngare ni wawili walionusurika katika ajali hiyo ya mafuriko, pamoja na wengine tisa wa familia ya Edward, licha ya kuachwa bila makazi.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages