
Rais Bashar al-Assad
Vikosi vya waasi vimeitangaza Syria kuwa "huru", vikisema rais "dhalimu" Bashar al-Assad ameondoka.
Ni mwisho wa enzi ya giza na mwanzo wa mpya, HTS inasema kwenye Telegram.
Watu waliofurushwa makwao au waliofungwa gerezani na utawala wa Assad wa nusu karne sasa wanaweza kurudi nyumbani, waasi wanasema.
Itakuwa "Syria mpya" ambapo "kila mtu anaishi kwa amani na haki itatawala," HTS inasema.
Rais wa Syria, Bashar al-Assad amepanda ndege na kuondoka mji mkuu Damascus kwenda kusikojulikana, shirika la habari la Reuters limeripoti hivi punde likiwanukuu maafisa wawili wakuu wa Syria.
Mfuatiliaji wa vita wa SOHR pia anasema ndege ya binafsi ambayo imeondoka kwenye uwanja wa ndege wa Damascus huenda ikawa imembeba Assad.
Wanajeshi wa serikali katika uwanja wa ndege waliondoka baada ya kuondoka kwake, ilisema.
Haya yanajiri huku wanajeshi wa waasi wakisema wameanza kuingia katika mji mkuu wa Syria.
Wafungulia wafungwa
Waasi wameripotiwa kuachia wafungwa kutoka kwenye gereza baya zaidi nchini Syria maarufu la Saydnaya, lililowahi kuelezewa na Umoja wa Mataifa kama "machinjio ya binadamu", ambapo maelfu ya wafuasi wa upinzani wanasemekana kuteswa na kunyongwa.

HTS ilitangaza kwenye Telegram kwamba wafungwa wameachiwa, na kuiita "mwisho wa enzi ya ukosefu wa haki" huko Saydnaya.
Video ambazo hazijathibitishwa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha watu wakitoka jela.
Chama cha Wafungwa na Waliopotea katika Gereza la Sednaya kilisema wafungwa walioachiwa walikuwa wakielekea Manin, mji ulio karibu na Damascus.
Chanzo: BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Waandishi wa habari Mara kushiriki kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
>>Rais Samia ateua na kubadilisha viongozi, Bashungwa apewa Wizara ya Mambo ya Ndani
>>Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kufanya ziara ya siku nne mkoani Mara
>>Wabunge wa Tanzania wapata ajali wakienda mashindano ya michezo Kenya
No comments:
Post a Comment