NAIBU Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita
Waitara, leo Mei 30,2020 ameungana na mamia ya waombolezaji katika
mazishi ya Aneth Batholomeo ambaye ni mama mzazi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya
PKM, Pastory Batholomeo Machage.
 |
| Naibu Waziri Waitara (wa pili kulia) na wananchi wengine katika mazishi hayo |
Mazishi hayo yamefanyika
nyumbani kwa marehemu Nyamongo na kuhudhuriwa na wananchi, viongozi wa serikali
na vyama vya sisasa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Akiongea katika mazishi
hayo, Naibu Waziri Waitara ametoa pole kwa familia ya Batholomeo
Machage kwa kuondokewa na mama yao.
 |
| Naibu Waziri Waitara akitoa salamu za pole kwa familia |
Waitara ametumia nafasi
hiyo pia kuonya kuwa serikali haitawavumilia wanasiasa wanaochochea migogoro
ya ardhi katika baadhi ya maeneo wilayani Tarime.
Amesema uchochezi huo
unaweza kusabbisha uvunjifu wa amani ambayo hivi sasa imetamalaki wilayani
humo.
 |
| Wakili Otieno Onyango (katikati mwenye miwani) akiwa na baadhi ya wananchi wa Nyamongo |
“Mimi kama mwenyeji wa
Tarime, kijana wenu na ambaye nimebahatika kuwa katika Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli, tunajua kumekuwepo na malalamiko
miaka ya nyuma ya ulipwaji wa fidia hapa Nyamongo, lakini Awamu ya Tano
imeanza kusimamia ulipwaji wa fidia hizo na hili katika ustaarabu wa kawaida
ni jambo la kumshukuru Rais Magufuli,” amesema Waitara.
 |
| Naibu Waziri Waitara akisaini kitabu cha rambirambi |
Naibu Waziri huyo wa
Tamisemi amewataka wananchi kupokea malipo hayo na kuwaomba wenye malalamiko
watumie njia sahihi kuyafikisha serikalini.
 |
Mkurugenzi wa kampuni ya PKM Pastory Batholomeo Machage
(wapili kutoka kulia) akipokea rambirambi kutoka kwa wanachama wenzake wa
kikundi cha Nyamongo Saving Group. Wakwanza kushoto ni kada wa CCM Nicodemus Keraryo
|
|
Habar za sauti ya Mara ni Moto hongeren sana kwa kazi nzur mnazozifanya mbarikiwe sana
ReplyDelete