NEWS

Wednesday, 21 August 2024

Makatibu wa Jumuiya za CCM Tarime watembelea Mara Online



CEO wa Mara Online News na Sauti ya Mara, Mugini Jacob (wa pili kulia) akimkabidhi Katibu wa Wazazi CCM Wilaya ya Tarime, Haji Ally Kiyanga "Baggio" nakala ya gazeti wakati yeye na wenzake walipotembelea ofisi za vyombo hivyo vya habari mjini Tarime leo Agosti 21, 2024.
-----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Katibu mpya wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, Haji Ally Kiyanga - maarufu kwa jina la Baggio, leo Agosti 21, 2024 ametembelea ofisi za Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara, akiwa amefuatana na makatibu wa jumuiya tofauti za chama hicho tawala.

Makatibu aliofuatana nao ni Nyasato Manumbu wa UWT Wilaya na Tito Masele wa UVCCM Wilaya ya Tarime.

Katika ziara hiyo, Baggio ameeleza kuridhishwa na jinsi vyombo hivyo vya habari vinavyotangaza masuala ya maendeleo katika mkoa wa Mara.

“Mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni kuonesha jinsi chama tawala - CCM kinavyotekeleza ilani yake kwa vitendo,” amesema Baggio katika mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mara Online News na Sauti ya Mara, Mugini Jacob.

Kwa upande wake CEO Jacob amewambia viongozi hao kuwa habari za maendeleo zinapewa kipaumbele katika vyombo hivyo vya habari.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages