NEWS

Wednesday 28 August 2024

MNEC Boghohe awasili Tarime kumwakilisha Mwenyekiti UWT CCM Taifa harambee ya kuchangia vitega uchumi vya UWT



MNEC Hellen Boghohe (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na viongoziwa UWT Mkoa wa Mara na wilaya ya Tarime leo Agosti 28, 2024. (Picha na Mara Online News)
---------------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Tarime

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hellen Boghohe amewasili katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kushiriki harambee ya kuchangia miradi ya vitega uchumi vya UWT.

Boghohe ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) CCM Taifa, anamwakilisha Mwenyekiti wa Kitaifa wa Umoja huo, Mary Chatanda katika harambee hiyo.

Mara baada ya kupokewa na viongozi wa CCM Wilaya ya Tarime, wakiwemo Mwenyekiti wa UWT Wilaya, Neema Charles na Katibu wa Chama Wilaya, Noverty Kibaji leo Agosti 28, 2024, MNEC Boghohe amekagua mradi wa ujenzi wa vibanda vya biashara vya chama hicho mjini Tarime.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages