NEWS

Saturday, 14 September 2024

Hatimaye mwanariadha Rebecca Cheptegei azikwa kijeshi nchini Uganda



 
Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza mashariki mwa Uganda kwa ajili ya mazishi ya mwanariadha wa mbio za marathon za Olimpiki Rebecca Cheptegei, ambaye alichomwa moto na aliyekuwa mpenzi wake na baadaye kufariki.

Dickson Ndiema alimshambulia kwa petroli Rebecca, chini ya wiki mbili zilizopita nje ya nyumba yake katika eneo jirani la kaskazini-magharibi mwa Kenya, karibu na alipokuwa anafanyia mazoezi.

Mauaji ya msichana huyo mwenye umri wa miaka 33, na tabia ya ukatili wa mwanaume huyo, yaliiacha familia yake ikiwa imefadhaika na kuwashangaza wengine wengi duniani.

Kifo chake kilionyesha ongezeko la viwango vya juu vya unyanyasaji dhidi ya wanawake nchini Kenya na ukweli kwamba wanariadha kadhaa wa kike wamekuwa waathiriwa katika miaka ya hivi karibuni.
Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria katika msiba wa Rebecca Cheptegei
---------------

Cheptegei amepokea heshima kamili za kijeshi katika mazishi hayo nchini Uganda, baada ya kuwa mwanajeshi huko.

Jeneza lake lilionekana likiwa limefunikwa bendera ya Uganda, huku mazishi yanaongozwa na viongozi wa eneo la Bukwo, wilaya ambayo alizaliwa Cheptegei na ibada ya mazishi kufanyika huko.

Waombolezaji walikaa kimya kwa muda wa dakika moja kutoa heshima zao kwa marehemu ,mwanariadha Cheptegei.
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages