Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele akiikabidhi Kewanja FC kombe la ubingwa wa Mahusiano Cup kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Ingwe wiki iliyopita. (Na Mpigapicha Wetu) |
--------------------------------------------
NA MWANDISHI MAALUMU
--------------------------------------
Ukifika Nyamongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara - ukataja maneno: Mahusiano Cup; wenyeji watakueleza haraka kwamba unazungumzia moja ya jitihada zinazofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kuboresha uhusiano wake na jamii inayouzunguka.
Mgodi huu ambao unaendeshwa na Kampuni ya Barrick Gold kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals, umekuwa ukibuni na kutekeleza mambo mbalimbali kwa hali na mali kwa manufaa ya wananchi.
Moja ya mambo ambayo mgodi huu umeanzisha na kudhamini ni mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana - yaliyopewa jina la Mahusiano Cup na kaulimbiu inayosema “Mahusiano Bora kwa Uwekezaji Endelevu.”
Mashindano haya si tu ni tukio la michezo, bali pia yanatajwa kama jukwaa muhimu la kujenga na kuimarisha uhusiano kati ya mgodi huu na jamii inayouzunguka.
Wananchi mbalimbali wakiwemo vijana wamezungumza na Gazeti la Sauti ya Mara kwa nyakati tofauti na kukiri kwamba mashindano ya Mahusiano Cup ambayo yanadhaminiwa na mgodi wa North Mara yamekuwa chachu ya kuboresha uhusiano baina ya pande hizo mbili.
Mgodi unatoa vifaa vya michezo na kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuwezesha mafunzo na usaidizi wa kitaaluma kwa vijana wanaoshiriki mashindano haya.
Kwa kushiriki katika mashindano haya kila mwaka, vijana wanapata fursa ya kuonesha na kukuza vipaji vyao vya michezo, kujenga afya zao kimwili na kiakili, kufahamiana, kujifunza ushirikiano na nidhamu, kubadilishana mawazo na hata uzoefu kwa upendo.
“Mashindano haya yamewezesha vijana wengi kuibua na kukuza vipaji vyao, na baadhi yao wameanza kufuatiliwa na timu zinazocheza ligi daraja la kwanza ngazi ya mkoa,” alisema mkazi wa kijiji cha Nyangoto, Ismail Hassan katika mazungumzo na gazeti hili wakati wa fainali ya Mahusiano Cup iliyochezwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Ingwe iliyopo Nyamongo, kilomita chache kutoka mgodi wa North Mara.
Iwe ni kupitia michezo, au shughuli za kiuchumi, mashindano haya yanahamasisha ushirikiano, ikiwa ni pamoja na kuwapa wananchi fursa ya kujifunza kutoka kwa wengine na kujenga jamii yenye umoja na mshikamano.
Aidha, mamia ya wananchi wanaokutanishwa na mashindano ya Mahusiano Cup wanapata pia fursa ya kuelimishwa jinsi mgodi unavyochangia maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.
Msemaji wa Timu ya Nyamwaga FC inayoshiriki ligi ya Mahusiano Cup, Emmanuel Sengeli anaushukuru mgodi wa North Mara akisema mashindano hayo yanasaidia kubadilisha tabia mbaya miongoni mwa vijana katika jamii inayouzunguka.
“Mgodi umefanya jambo la maana sana kuanzisha mashindano haya kwa sababu yanawezesha vijana kufunguka akili na kuamua kuacha vitendo viovu vikiwemo vya kwenda kuvamia mgodi na kuiba mawe ya dhahabu,” anasema Sengeli.
Hata hivyo, kijana huyu anashauri mgodi huu kuangalia uwezekano wa kuanzisha na kudhamini mashindano mengine ya michezo na burudani kama vile ya mpira wa pete na kikapu, riadha na muziki ili kuwezesha vijana wengi zaidi kujitokeza kuibua na kukuza vipaji vyao katika eneo hilo.
Naye mkazi wa kijiji cha Kewanja, Modester Mwita anasema mashindano haya yanachangia kuchangamsha biashara mbalimbali miongoni mwa jamii inayozunguka mgodi wa North Mara.
“Kutokana na mashindano haya kuvutia na kuwaleta pamoja watu wengi, biashara mbalimbali kama vile vinywaji baridi, matunda na migahawa ya chakula katika maeneo yaliyo jirani na viwanja vinavyotumika huwa zinachangamka siku za mechi,” anasema Modester.
Fainali ya mashindano ya Mahusiano Cup ya mwaka huu wa 2024 ilipeleka kicheko kwa Timu ya Kewanja FC ambayo ilitwaa ubingwa kwa mara ya tano mfululizo - kwa kuichapa Nyamwaga FC mikwaju ya penalti 3-1, baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.
Mgeni rasmi katika fainali hiyo, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele aliikabidhi Kewanja FC kombe la ubingwa huo, mbele ya Meneja Mkuu (GM) wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko, miongoni mwa viongozi wengine.
DC Gowele aliupongeza mgodi wa North Mara kwa kuanzisha na kudhamini mashindano hayo, huku akiahidi kwamba serikali itaendelea kuupa ushirikiano katika kuyaendeleza, ili kuboresha zaidi uhusiano na jamii inayouzunguka.
Awali, GM Lyambiko alimweleza kiongozi huyo wa serikali kwamba mgodi wa North Mara unatumia mashindano hayo kama moja ya njia za kuimarisha zaidi uhusiano kati ya mgodi huo na jamii inayouzunguka, sambamba na kujadili changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa manufaa ya pande zote mbili.
Alisema Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick Gold, Dkt Mark Bristow alishaahidi kugharimia ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo katika mji wa Nyamongo, ili kuhamasisha zaidi michezo kwa vijana katika maeneo yanayozungu mgodi huo.
Kwa kuanzisha na kuendelea kudhamini mashindano ya Mahusiano Cup, mgodi wa North Mara unadhihirisha dhamira yake njema ya kujenga na kuimarisha uhusiano na jamii inayouzunguka, ili pia kuwezesha shughuli zake za uchimbaji madini kuendelea bila vikwazo vya kuvamiwa na makundi ya watu wanaopora mawe ya dhahabu na kuharibu miundombinu yake.
“Hatua hii inastahili kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo kwani ni njia bora ya kujenga mustakabali mzuri kwa wote, ambapo mgodi na jamii wanaweza kushirikiana kutatua changamoto zilizopo kwa faida ya wote,” anasema mkazi wa kijiji cha Matongo, Pius Matinde.
Kwa ujumla, mashindano ya Mahusiano Cup yanabaki kuwa mfano bora wa jitihada zinazofanywa na mgodi huu katika kujenga na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati yake na jamii inayouzunguka kwa manufaa ya pande zote mbili.

UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Esther azindua Matiko Foundation, agawa misaada lukuki, RC Mara ampongeza
>>FZS, Grumeti Fund win accolades for rhino conservation
>>HABARI PICHA:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa na wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chifu Zulu ya mjini Songea, mkoani Ruvuma, wakiimba wimbo kuhusu matumizi ya kompyuta jana.
No comments:
Post a Comment