NEWS

Sunday, 1 September 2024

Mkurugenzi Goldland Hotel ashiriki chakula cha pamoja na wanafunzi wa Moregas



Waliosimama nyuma - kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Moregas English Medium, Cosmas Wangwe, Mkurugenzi wa Goldland Hotel, Simon Mseti Wangwe, mfanyabiashara maarufu Peter Zakaria na wadau wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule hiyo mjini Tarime jana.
----------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Tarime

Mkurugenzi wa Goldland Hotel, Simon Mseti Wangwe ameandaa na kushiriki chakula cha pamoja na wanafunzi 60 wa Shule ya Msingi ya Moregas English Medium iliyopo Sirari wilayani Tarime, Mara.

Wanafunzi hao ni ambao wiki ijayo wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu Darasa la Saba mwaka huu wa 2024.

Hafla hiyo ya chakula cha pamoja ilifanyika Goldland Hotel mjini Tarime jana mchana, lengo likiwa ni kuhamasisha suala la taaluma kwa wanafunzi hao.


Mkurugenzi Wangwe alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao za elimu.

“Nawashukruni kufika na kula chakula pamoja. Mshike masomo, watoto wa kike msidanganyike - usikubali kuacha shule. Nimewaita hapa kwa makusudi, nataka muwe mfano kama Goldland huyu [mwenyewe Wangwe], kama Zakaria [mfanyabiashara maarufu wa mjini Tarime], na mazingira ya sasa lazima msome ndio mfanikiwe,” Wangwe aliwambia wanafunzi hao na kuongeza:

“Mama Samia Suluhu Hassan [Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania] kaboresha mazingira ya kujifunzia, popote utakapochaguliwa kwenda utapata shule ya kusoma, usiku na mchana anatengeneza mazingira ambayo hayana gharama kubwa mpaka vyuo vikuu.”

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau kadhaa wa maendeleo, akiwemo Peter Zakaria na Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Moregas English Medium, Cosmas Mseti ambaye alimshukuru Mkurugenzi Wangwe kwa namna ambavyo anajitolea na kushiriki katika uhamasishaji wa elimu kwa watoto.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages