NEWS

Tuesday 17 September 2024

Mwenyekiti Halmashauri ya Serengeti atembelea ofisi za Gazeti la Sauti ya Mara



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa CEO wa Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara, Jacob Mugini - alipotembelea ofisi za vyombo hivyo vya habari mjini Tarime jana.
------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma jana alitembelea ofisi za Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara mjini Tarime, na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa vyombo hivyo vya habari, Jacob Mugini.

Mazungumzo yao yalihusu namna nzuri ya kushirikiana katika kutangaza habari za maendeleo za halmashauri hiyo yenye utajiri mkubwa wa wanyamapori.

"Halmashauri yetu ya Serengeti ni ya kitalii na tunapenda kutangaza habari positive (chanya) za maendeleo," alisema Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe kwa tiketi ya chama tawala - CCM.

Kwa upande wake Mugini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara, alisema vyombo hivyo vya habari vinazipa kipaumbele makala na habari za maendeleo, zikiwemo za uhifadhi na maendeleo endelevu ya jamii.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages