NEWS

Thursday, 19 September 2024

Polisi: Boniface Jacob hajatekwa, tumemkamata kwa makosa ya jinai


Boniface Jacob “Bon Yai”

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Jeshi la Polisi limesema limemkamata na kumshikilia mkazi wa Mbezi kwa Msakuzi jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob maarufu kwa jina la “Bon Yai” kutokana na tuhuma za makosa mbalimbali ya jinai.

“Hivyo, wananchi wapuuze uongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa,” Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, DCP David Misime alisema jana Septemba 18, 2024 kupitia taarifa yake kwa umma.

Boniface Jacob amewahi kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages