NEWS

Wednesday 4 September 2024

Rais Samia kushiriki mkutano wa ushirikiano wa China na Afrika



Rais Dkt Samia Suluhu Hassan (mbele) akipokewa kwa shangwe alipowasili jijini Beijing, China jana.
-----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan aliwasili jijini Beijing jana kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Tisa wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

Aprili 26 2024, Tanzania na China zilitimiza miaka 60 ya mahusiano ya kidiplomasia na kimkakati yenye tija kwa pande zote mbili.

“Kama ilivyokuwa ndoto ya waasisi wetu, jukumu letu ni kuhakikisha tunaendeleza mahusiano haya yaweze kuleta tija zaidi hasa katika maendeleo ya sekta muhimu za uchumi wetu,” alisema Rais Samia.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages